The House of Favourite Newspapers

A-Z aliyechinja mpenzi, watoto

0

IMG_8393

Mtoto baada ya kufanyiwa unyama huo.

Na Stephano Mango, SONGEA

MAJONZI! Bado ni tukio baya sana kutokea katika Kijiji cha Kikunja, Kata ya Ndongosi, Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma ambapo mkazi wa kijiji hicho, Amani Hyela (42), anadaiwa kuwaua kwa kuwachinja kwa panga mpenzi wake, Ester na watoto wake wawili kisa kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo la kutisha lilijiri saa saba usiku wa Novemba 28, mwaka huu ambapo Amani anadaiwa kuwaua watu hao kwa kuwachinja na kuwakata na panga sehemu mbalimbali za miili yao na baadaye yeye kujijeruhi kwa kujikata shingoni na kujisababishia majeraha makubwa.

Kama ada ya Gazeti la Uwazi, mara baada ya kupata taarifa za ukatili huo lilifika eneo la tukio na kujikusanyia maelezo kutoka kwa mashuhuda na majirani wa eneo hilo.

“Mimi ni jirani wa marehemu Ester, siku hiyo usiku nilishtuliwa na kelele za watu. Nikatoka nje na kubaini kuwa, kelele hizo zilikuwa zikitokea kwenye nyumba hii. Kufika nikakuta watu wengi, mtuhumiwa yuko chini anavuja damu.

“Niliulizia kulikoni, nikaambiwa Amani amevamia nyumbani hapo na kumchinja Ester na watoto wake wote. Nilishangaa sana. Ester nilimwona mchana wake, alikuwa wa afya njema kabisa. Huu ni ukatili. Dunia ya sasa unyama umeongezeka sana. Si Tanzania tu. Kila mahali unyama, ukatili,” alisema jirani mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.

IMG_8387

Mama akiwa amelala chini baada ya kufanyiwa kitendo hicho cha kinyama.

Shakira Moyo, mkazi wa kijiji hicho na mama mzazi wa marehemu Ester aliliambia gazeti hili kuwa, ni unyama mkubwa ambao haujawahi kutokea kwenye kijiji hicho na kwamba anamfahamu Amani ambaye ni mlalamikiwa.

Shakira alisema mauaji hayo yamemuumiza sana kwa vile yamempotezea mwanaye na wajukuu wawili ambao kimsingi hawana hatia yoyote katika wivu wa kimapenzi wa wazazi wao lakini wamekatishwa uhai wao.

Alisema kuwa marehemu Ester alikuwa na watoto wawili ambao walizaliwa kwa baba tofauti (si Amani) lakini kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Ester akawa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo.

“Ester na Amani waliishi kama mume na mke na baadaye waliachana kufuatia Ester kusema kuwa ameokoka na kwamba hataki tena masuala ya mapenzi (nje ya ndoa) jambo ambalo lilipingwa na mwanaume,” alisema Shakira.

picha2

Mtuhumiwa akiwa amefungwa kamba.

Aliongeza kuwa, kitendo hicho ndicho kilichomfanya Amani kuamua kuchukua uamuzi huo uliosababisha vifo vya watu watatu na yeye mwenyewe kujijeruhi ambapo pia alinusurika kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira.

“Inaonekana Amani aliamini Ester anamkataa kwa kuwa ana mwanaume mwingine ndiyo maana aliona bora amtoe uhai na kuwamaliza na watoto na yeye ajiue. Naamini amejijeruhi lengo lilikuwa kujiua,” alisema mwanamke huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Mihayo Msikhela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

IMG_8412Alisema siku ya tukio, baada ya taarifa kufika kituoni, polisi walikwenda eneo husika na kukuta watu hao wameshafariki dunia huku mtuhumiwa akiwa amejichinja koo akiwa amefungwa mikono kwa waya.

Alisema mtuhumiwa akiwa anavuja damu, alikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambako amelazwa akipatiwa matibabu huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Leave A Reply