The House of Favourite Newspapers

Abby Cool Afungukia Shindano la Mfalme wa Rhymes, Alivyokutana na Shigongo – Video

0

KATIKA kipindi cha ‘KATAMBUGA’ leo Novemba 10, amesikika  mdau mkongwe wa muziki, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ ambaye ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, kuhusiana na masuala mbalimbali ya muziki ikiwemo kuanzishwa kwa Shindano maarufu la Mfalme wa Rymes, shoo ya kwanza ya Diamond kushuka na Helkopta Dar Live na safari yake hadi kukutana na Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Mhe. Eric Shigongo.

 

ABBY COOL ALIVYOKUTANA NA SHIGONGO

“Zamani wakati wa sikukuu tulikuwa tunapiga picha kwenye familia za watu, tofauti na sasa hivi ambapo kuna photo studios, Hivyo mimi nilijichanga nikanunua kamera nikawa napiga picha kwenye familia na maeneo mbalimbali ya events zikiwemo za burudani.

 

“Siku moja nikaona nipeleke picha zangu nilizokuwa nimepiga za matukio ya burudani Global Publishers, ofisi zilikuwa karibu na maeneo ya Maktaba na Global ndio walikuwa na Gazeti linalobamba kwa burudani la KIU, nilipofika pale sikumkuta shigongo lakini nilikuta watu wengine nikawaeleza wakapokea picha zangu zikatumika kwenye gazeti.

 

“Kuanzia hapo nikawa nikipiga picha za matukio nawaletea, zinatumika kwenye gazeti, siku moja nilipoleta nikamkuta Shigongo, tukazungumza, kwa kuwa hawakuwa na mpiga picha rasmi, mimi ndio nikawa mpiga picha wao.

 

“Na ili kumfahamu msanii yeyote maarufu ilikuwa lazima umsome kwenye gazeti hivyo nikaendelea mpaka ikafika wakati sasa nikawa nahusishwa kwenye kuandaa gazeti mwanzo hadi mwisho, baadaye Gazeti la Kiu likaondoka mikononi mwetu tukaanzisha Gazeti letu la Ijumaa ambalo mpaka leo lipo.

 

UNAWEZAJE KUZUIA STRESI ZA NYUMBANI ZISIFIKE KAZINI?

“Uongozi ni hekima na unatakiwa uwe na vitu ambavyo huwezi kuvipata shuleni ama darasani, Kikubwa unapaswa ujue namna ya ku-react wakati jambo lolote linapotokea ili usiharibu.

 

“Linapotokea jambo reaction yako inaweza kutengeneza au kuharibu jambo, hivyo ukiwa kama kiongozi lazima ujue namna ya kuji-control na hicho ndicho kipimo cha uongozi kiongozi ni yule anayeweza kukabiliana na changamoto au tatizo linapotokea.

 

KUHUSU UPIGAJI PICHA
“Tasnia ya upigaji picha ni inakwenda inakuwa sana, kuanzia sisi tulipoikuta mpaka leo ilipofikia imepiga hatua kubwa sana, angalia ubora wa picha kizazi hiki cha kupiga picha kuna maboresho makubwa sana kuanzia kwenye digital camera zenyewe, computers na software zinazotumika na teknolojia kwa ujumla ni tofauti kabisa na enzi zetu.

 

KUHUSU DJ JOHN DILINGA

“Dj JD tunafahamiana muda mrefu sana, kwenye kazi zetu hizi za burudani na habari tumekutana mara nyingi sana, Sisi kama kama kampuni tulifanya mashindano mengi sana ya sanaa.

 

“Kuna shindano la ku-rap la Mkali wa Rhymes ambalo tulianzisha, mimi pamoja na Dj JD tulikuwa majaji pamoja na wengine, kwa hiyo mahusiano yetu na DJ uliimarika sana, alikuwa akitoka kwake anakuja kila weekend tunafanya kazi, hivyo ni mtu wetu wa karibu sana tangu kitambo.

 

“Mara nyingi amenialika Club Legend, kutokana na majukumu ya ofisi na kifamilia sijapata nafasi, lakini ipo siku nitakwenda, Anapiga ngoma zile zenyewe hasa kwetu sisi wahenga, zinabamba sana” amesema Abby Cool,  ambaye ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, mdau wa masuala ya burudani na mpiga picha mkongwe.

<\center>

Leave A Reply