The House of Favourite Newspapers

ACACIA Yataka Mazungumzo na Serikali ya Tanzania

KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya Acacia inataka mazungumzo na serikali ili kupata suluhu ya mgogoro wa kodi uliopo hivi sasa baada ya kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya Barrick kununua mali za Acacia ikiwemo migodi mitatu iliyopo nchini.

Barrick Gold inamiliki asilimia 64 ya hisa za Acacia na kwa sasa inajiandaa kununua asilimia 36 ya hisa zilizobaki.

Ununuzi huo wa hisa umesogezwa mbele hadi Julai 9, 2019, wakati jitihada za kufanya mazungumzo na serikali zikiendelea.

Serikali  ilizuia shehena ya makinikia yaliyokuwa yako mikononi mwa Acacia hadi itakapolipa deni la kodi la kiasi cha zaidi ya Sh. trilioni 436.

Comments are closed.