The House of Favourite Newspapers

ACB, SAVING BANK NA TAMFI KUTOA ELIMU YA KIBENKI

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano (ACB) Dora Saria akifungua kikao hicho.

BENKI inayokua kwa kasi ya Akiba Commercial Bank (ACB) kwa kushirikiana na taasisi za Saving Bank na shirikisho la asasi zinazotoa huduma ndogondogo za fedha (TAMFI) wameingia mkataba wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa uwekaji na utunzaji wa fedha benki, nidhamu ya fedha, umuhimu wa akiba na mambo mengine.

Akizungumza baada ya kutiliana saini taasisi  za ACB, Saving Bank na TAMFI, Meneja Mkuu na Uendeshaji wa ACB, Juliana Swai, alisema elimu hiyo italolewa zaidi kwa watoto kwa maana elimu ya nidhamu ya fedha ni muhimu inapotolewa kuanzia utotoni ambapo ni vyema zaidi watoto wanapokuwa nayo kwa maana jambo linapofundishwa kuanzia utotoni linadumu akilini.

Huduma hiyo inatarajiwa kutolewa nchi nzima, mijini na vijijini.

Matukio Katika Picha:

Maofisa hao wakitiliana saini wakati wakiingia mkataba huo.
Meneja Mkuu, Uendeshaji, Juliana Swai (kulia) akikabidhiana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa shirikisho la sasi zinazotoa huduma ndogondogo za fedha, (TAMFI) Winnie Terry.
Mkurugenzi Mkazi wa Saving Bank, Stephen Noel (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu Uendeshaji wa ACB, Juliana Swai.
Maofisa hao wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika zoezi hilo.

 

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL  

Comments are closed.