The House of Favourite Newspapers

Wanakijiji Waamua Kufuga Pweza – Video

WANAKIJIJI wa Songosongo, Kata ya Songosongo, Kilwa, mkoani Lindi,  wameishukuru serikali kwa kuwaletea mpango wa uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa bahari ujulikanao kama Mwamba Darasa uliofadhiliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la WWF.

 

Mpango huo wa Mwamba Darasa uliokuwa umefungwa kwa kipindi cha miezi mitatu ili kuruhusu uzalishaji wa pweza, umefunguliwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) hiyo Haji Mbaruku.

 

Mbaruku amesema kuwa wananchi wa Songosongo wanatakiwa kutuza mazingira ya eneo hilo huku akiwataka viongozi wa Shirika la Usimamizi wa Raslimali za Uvuvi Baharini (BMU) kuacha tabia ya ubaguzi, kwa kutoa vibali kwa kufuata itikadi za vyama na badala yake waige mfano wa Rais John Magufuli kwa kuleta maendelo bila kujali itikadi za vyama.

Comments are closed.