The House of Favourite Newspapers

Makonda: Acheni Chokochoko Za Kuwasumbua Wabunge Na Madiwani, Waacheni Wafanye Kazi Zao

0
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wanachama wa chama hicho kuacha kufikiria nafasi za udiwani, ubunge kwa sasa badala yake wawaunge mkono waliopo katika nafasi hizo.

Hayo yameelezwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda katika mkutano wake na waandishi wa habari kutoa tathmini ya robo mwaka ya utendaji kazi wa chama hicho, katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam.

Amesema CCM inawatambua viongozi waliopo na inawaunga mkono, hivyo imewataka wanachama wake kuacha kuwapa presha viongozi waliopo kwani wakati muafaka ukifika watawania nafasi hizo.

“CCM inatoa rai kwa watu walio na shauku ya kutaka Majimbo na Udiwani, sasa CCM inasema chokochoko zote ziachwe mara moja, wabunge wapewe nafasi ya kufanya kazi zao kama ulivyo utaratibu na katika hili nitoe mfano mimi niligombea ubunge Kigamboni nikashindwa na akateuliwa mgombea wa Chama kwa kura za maoni na mimi nikakubali kushindwa na kuacha na sijawahi tena kwenda kigamboni nimemuacha mbunge afanye kazi zake”

“Acheni kuwanyima utulivu viongozi wetu, waacheni wafanye kazi zao, acheni kuwachafua huko kwenye magroups ya whatsapp, tuwape ushirikiano kwasababu kumuyumbisha maana yake unayumbisha utekelezaji wa Ilani ya CCM, Marufuku kufanya hivyo” amesema Makonda.

Leave A Reply