The House of Favourite Newspapers

ACT Yaanika Usiyoyajua Kuhusu Maalim Seif – Video

0

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema kuwa vuguvugu la kumng’oa Maalim Seif kutoka Chama cha Wananchi CUF kuelekea ACT lilianza mara tu baada ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

 

Hayo yamesemwa leo na Ado Shaibu ambaye ni Katibu Mkuu ACT Wazalendo leo Ijumaa, Machi 5, 2021 wakati akizungumza katika Mahojiano na kipindi cha #frontPage kinachoruka kupitia Global Radio.

 

“Ujio wa Maalim Seif ACT ulianza kupikwa baada ya uchaguzi wa 2015, Zitto alizungumza maneno mazito pale Mbagala Zakhiem akionyesha msimamo mkubwa wa kuitetea Zanzibar, ambayo yaliwavuta akina Maalim.

 

 

Hata uchaguzi wa marudio Zanzibar 2016 tulikataa kushiriki, Makamu Mwenyekiti Zanzibar akawepa mtu kinyemela, tukamvua uongozi. Hatukuwa UKAWA wala hatukuwa na matumaini kushinda uchaguzi ule lakini chama kilichukua maamuzi magumu ambayo hayajawahi kufanywa na chama, hii iliwaonyesha akina Maalim kuwa chama hiki kimedharimia.

 

 

“Nguvu yetu kule Zanzibar ina maana kubwa kwa Bara, maeneo yalikuwa kambi ya CUF kuanzia Kusini mpaka Pangani sasa hivi ACT Wazalendo ndiyo ina nguvu maeneo hayo na ukiyafanyia utafiti utagundua kama hatujashinda diwani ama mbunge sisi ni wa pili.

 

 

“Maalim Seif kisima cha mafanikio yake kina kina kirefu sana, huwezi kukimaliza kwa muda mfupi. Kama ningebahatika kuishi na miaka mitano, basi ningepata shahada na shahada na shahada ya uongozi.

 

 

“Maalim Seif alikuwa akitenga muda kuongea na kujibu meseji za viongozi waandamizi na wanachama wa kawaida, si kutoa tu michango alikuwa anaibuka kwenye ndoa za wapiganaji wake wa kawaida kabisa, alikuwa na heshima kwa kiwango kikubwa, alikuwa mkweli na si mnafiki,” amesema Ado Shaibu.

 

Leave A Reply