The House of Favourite Newspapers

Ado Sahibu: Chimbuko la ACT Wazalendo ni Chadema – Video

0

 

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema kuwa chimbuko la chama hicho kwa asilimia kubwa limetokaana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndiyo maana vyama hivyo vimekuwa na ushirikiano mzuri katika harakati zao za kisiasa na kidemokrasia.

 

Hayo yamesemwa leo na Ado Shaibu ambaye ni Katibu Mkuu ACT Wazalendo leo Ijumaa, Machi 5, 2021 wakati akizungumza katika Mahojiano na kipindi cha #frontPage kinachoruka kupitia Global Radio.

 

 

“Mwenezi kazi yake ni kuki-brand na kukisemea chama, katibu mkuu ni injini ya chama, watu wanalala usingizi wakiamini chama kipo salama chini ya katibu mkuu. Kila jambo linalohusu chama linaratibiwa na katibu mkuu, huwezi kulala.

 

 

“Lazima tukubali kuwa chimbuko la ACT Wazalendo ni Chadema, kwa sababu Zitto Kabwe alikuwa kiongozi mwandamizi ndani ya Chadema, pia baadhi ya watu walioanzisha ACT Wazalendo walitoka Chadema, kwa hiyo ilikuwa lazima tushirikiane.

 

 

“Watu waliofanya kazi kubwa ya kumaliza tofauti kati ya Chadema na ACT ni Mbowe na Zitto Kabwe. Wakati Mbowe anatuhumiwa na RC wa Dar kuwa anajihusisha na madawa ya kulevya, Zitto kwa mara ya kwanza Zitto alikuwepo kwenye press ya Mbowe na akamtetea.

 

 

“Kuna wakati tunapishana kwa sababu ya itikadi lakini kuna wakati tunakuwa pamoja, haya mambo yanakuwepo kwenye siasa. Wapo baadhi ya viongozi waliondoka ndani ya Chama akiwemo mama Anna Mghwira, Dkt. kitila Mkumbo na bado tuliheshimu maamuzi yao na kuwatakia kila la kheri, hata Bernard Membe pia hivyo hivyo.

 

Leave A Reply