The House of Favourite Newspapers

Afikishwa Mahakamani kwa Kujipachika Cheo cha Msigwa wa Ikulu

0

mahakamani

Mfanyabiasha Ramadhani Athumani Juma maarufu kama Elias Jeremiah Mazimbaka amefikishwa mahakamani  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar akikabiliwa na shitaka la kujitambulisha kuwa yeye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa.

Akisoma hati ya shitaka hilo, Wakili wa Serikali, Jacqline Nyantori alidai kuwa kati ya Juni 28 na Julai 4, mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya alijitambulisha kama Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu kwa Ladslaus Matindi.

Amedai kuwa mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo katika kipindi hicho kwa lengo la kujaribu kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Mshtakiwa alikana shitaka na upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado haujakamilika,

Mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya sh 1 milioni. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 23 mwaka huuu na akitupwa rumande.

 

NA: MWANDISHI WETU

Leave A Reply