The House of Favourite Newspapers

Afisa TFF Amshtaki CEO Simba Polisi

0


AFISA wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF Jacqueline Kamwamu amemshataki Polisi Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez.

Mashtaka hayo yamefunguliwa katika kituo Kikuu Cha Polisi Jijini Dar Es Salaam.

Siku ya Alhamisi ya Januari 20, Barbara alipokea wito wa kufika kituoni hapo ambapo baada ya kufika aliwekwa ndani kwa saa nane kisha kusomewa shtaka lake.

Shtaka linalomkabili Barbara ni kutoa lugha isiyopendeza kwa Afisa wa TFF Jacqueline Kamwamu ambae alimzuia asiingie Uwanjani katika eneo la VIP na Watoto wadogo siku ya December 11 2021 katika mchezo kati ya Yanga na Simba.

Leave A Reply