The House of Favourite Newspapers

Nape Nnauye Atua Airtel, Awahakikishia Ushirikiano

0
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza na uongozi wa kampuni ya simu ya Airtel alipofanya ziara yake makao makuu ya Airtel leo. Mheshimiwa Nape katika mazungumzo hayo alipata fursa ya kusikiliza mipango endelevu ya Airtel, changamoto zinazowakabili kisha Mh, Waziri Nape alielezea mwelekeo wa serekali katika kusimamia sekta ya mawasiliano nchini kwa lengo la kuwafaidisha zaidi watanzania pale wanapotumia huduma za mawasiliano.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi, Beatrice Singano akielezea waandishi wa habari kufurahishwa kwa Airtel na ujio wa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Nape Nnauye mara baada ya Waziri huyo kutembelea makao makuu ya Airtel leo kwa lengo la kuendeleza mahusiano kati ya serikali na watoa huduma za mawasiliano.
…Nape Nnauye akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Airtel Tanzania Bw, Dinesh Balsingh (kati) na Mkurugenzi wa Airtel anaemaliza muda wake Bw, George Mathen alipofanya ziara yake makao makuu ya Airtel leo.

Airtel tunakushukuru sana Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Nnauye kwa utayari wako na serikali wakushirikiana nasi kuwahudumia watanzania. Alisema Mkurugenzi wa mawasilaino Airtel.

Leave A Reply