The House of Favourite Newspapers

Zaidi ya Nyaraka 300 za Siri Zakutwa Kwenye Makazi ya Trump

0
Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump

SERIKALI ya Marekani imekuta zaidi ya nyaraka 300 zenye alama ya siri nzito za serikali ya nchi hiyo, zikiwa kwenye makazi ya Rais wa zamani, Donald Trump huko Florida.

 

Miongoni mwa nyaraka zilizokutwa ni pamoja na nyaraka kutoka Shirika la Ujasusu (CIA), Usalama wa Taifa (NSA) na Shirika la Upelelezi wa Ndani (FBI).

 

Taarifa hii imetolewa Agosti 22, 2022 katika gazeti la

New York Times, lililonukuu vyanzo mbalimbali viliyoarifiwa kuhusu suala hilo.

Nyaraka 300 za siri zimepatikana katika makazi ya Donald Trump

Gazeti hilo limesema kuwa Taasisi ya Kitaifa ya utunzaji wa nyaraka January mwaka huu, iligundua seti ya kwanza lililokuwa na zaidi ya nyaraka 150 zenye siri nzito.

 

Mmamo Juni mwaka huu, wasaidizi wa Trump waliipatia Wizara ya Sheria seti ya pili huku seti ya tatu ikigunduliwa na FBI walipovamia makazi ya Trump mwanzoni mwa  mwezi huu.

FBI walifanya upekuzi hivi karibuni kwenye makazi ya Donald Trump

Mapema jana, Trump aliiomba mahakama ya shirikisho kuwazuia FBI kwa muda ili kupitia nyaraka ilizozikamata Agosti 8, 2022, kwenye makazi yake huko Mar-a-Lago hadi kutakapoteuliwa msimamizi maalumu wa kusimamia zoezi hilo.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave A Reply