The House of Favourite Newspapers

African Sports hawapigi kura

0

AFRICAN Sports imesema haina fedha za kuwasafirisha wachezaji wake kutoka Mbeya kwenda Tanga kupiga kura kisha kurejea tena mkoani humo kucheza na Prisons Alhamisi ijayo.

Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unafanyika kote nchini kesho Jumapili ikiwa ni fursa ya wananchi wa Tanzania kuchagua viongozi wao.

Makamu Mwenyekiti wa African Sports, Ahmed Bozinia aliliambia Championi Jumamosi kuwa, kikosi chao kipo Mbeya kikisubiri mechi dhidi ya Prisons, Alhamisi ijayo na wachezaji hawatapiga kura kesho.

“Wachezaji wetu walijiandikisha Tanga, lakini hatuna bajeti ya kwenda Tanga kupiga kura na kurudi Mbeya tena kwa ajili ya mechi. Tumeona ni heri kupoteza upande mmoja kwa ajili ya masilahi ya upande mwingine.

“Alhamisi tuna mchezo na Prisons jijini Mbeya City, hivyo tumeona tuusubirie hukuhuku ili kupunguza gharama,” alisema Bozinia ambaye timu yake ilifungwa bao 1-0 na Mbeya City Jumatano iliyopita.

Leave A Reply