The House of Favourite Newspapers

Afrika Kusini Yasasema Haina Mipango ya Kujiondoa kwenye Mkataba wa ICC kwa Ajili ya Putin

0

Ofisi ya rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaposa ametoa taarifa kwamba nchi yake haina mipango ya kujiondoa kwenye Mkataba wa Roma kuhusu kuanzishwa na mchakato wa mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) kinyume na kauli aliyozitoa mwenyewe rais Jumanne.

Mwezi Agosti kikao cha ZRICS kinatarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini, na kwa hali ilivyo sasa rais wa Urusi anapaswa kukaribishwa.

Afrika Kusini inaitambua kisheria mahakama ya The Hague, ambayo ilitoa waranti ya kumkamata Vradimir Putin, na atatakiwa rasmi kutekeleza waranti (hatahivyo, hakuna vikwazo vinavyotolewa kwa wasiotekeleza waranti).

Ofisi ya rais inadai kwamba chama tawala cha African National Congress (ANC) kilikosea katika mazungumzo . “Ofisi ya rais inataka kuweka wazi kwamba, Afrika Kusini bado imesalia kuwa mwanachama wa Sheria ya Roma… Hii inafuatia kutokamilika kwa kauli katika mazungumzo kwa vyombo vya habari yaliyofanywa na chama cha ANC,” ilieleza taarifa iliyotolewa usiku.

MSANII ALIYEANGUKA CHOONI kwa SHILOLE AFUNGUKA SHISHI KUMUWASHIA MOTO – “DIAMOND ALINIAMBIA NIIMBE”

Leave A Reply