The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Akutana Na Mtoto Hamimu Mwenye Matatizo Ya Ngozi, Ikulu Jijini Dar

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera. Mtoto huyo Hamimu alifika Ikulu kwa ajili ya kumshukuru Mhe. Rais kwa msaada aliompatia wa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. Rais alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa Ziara yake Nyakanazi Mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu baada ya kuhangaika kwa muda mrefu.

Rais Samia Suluhu Hassan, leo April 26, 2023 amekutana na kuzungumza na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) ikulu jijini Dar es Salaam.

Mtoto Hamim mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera amefika ikulu kwa ajili ya kumshukuru Rais Samia kwa msaada wa matibabu aliompatia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Rais alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa Ziara yake Nyakanazi Mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu baada ya kuhangaika kwa muda mrefu.

Rais Samia akiwa kwenye mazungumzo na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye alikuwa na shauku kubwa ya kumuona Rais Samia. Pichani mtoto huyo akiwa haamini macho yake mara baada ya kugundua kuwa aliyekuwa anazungumza naye ni Rais Samia, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumshukuru kwa msaada aliompatia wa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Rais Samia akimkaribisha Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaka wa mtoto huyo Saddam Mustapha Baranyikwa.
Leave A Reply