The House of Favourite Newspapers

Agizo la JPM Kuhusu Vyoo Soko la Kibiti Laanza Kutekelzwa – Video

0

Ikiwa ni siku chache Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania kusimama na kuzungumza na wakazi wa wilaya ya kibiti wakati akitoka kwenye maziko ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa mkoani Mtwara na kuelezewa changamoto ya huduma ya choo katika soko na stendi ya mabasi wilayani kibiti ujenzi wa vyoo umeanza na upo katika hatua za nzuri.

 

Global TV Online imefika katika soko hilo na kujionea namna ujenzi unavyoendelea na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo Homboka,Hamis Kitambulilo na Pili Kinjinje na kuelezea walivyoona utekelezajo wa agizo la Raisi Magufuli.

 

Abdalah Mn’goi nimwenyekiti wa soko la kibiti ameshukuru kwa hatua hiyo ya ujenzi wa choo hicho ambao ilikuwa kero kwao.

 

Ujenzi wa vyoo hivyo unatakiwa kukamilika kwa muda wa wiki moja kwa maagizo ya mheshimiwa Rais ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.

 

Leave A Reply