The House of Favourite Newspapers

Aguero Alalamikia Kunyimwa Pasi Uwanjani

0

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Muargentina  Sergio Kun Aguero,  amelalamikia uchoyo wa pasi kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo, katika  mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa jana usiku Machi 16, dhidi ya Borussia Monchengladbach na kuibuka na ushindi  mabao 2-0 kwenye dimba la Ettihad, nchini Uingereza.

 

Aguero ambaye aliingia dakika ya 75 kuchukua nafasi ya Bernardo Silva, alishindwa kupiga hata shuti moja ambalo lililenga lango hatua iliyopelekea kupeleka shutuma hizo za  kwa mastaa  wenzake ndani ya kikosi hicho.

 

Matokeo hayo yameipeleka City kwenye hatua ya robo fainali  ya michuano hiyo mikubwa barani ulaya.

 

Kwa kipindi kirefu msimu huu 2020/21  Kun Aguero alikuwa nje akisumbuliwa na majeraha na hii ikiwa ni mechi yake ya pili tangu arejee uwanjani.


Tukio hili limeongeza uvumi kuwa huena yupo mbioni kujiunga na rafiki yake mkubwa Lionel Messi katika klabu ya Fc Barcelona, mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huu na kocha Pep Guardiola anaonekana kutokuwa kwenye mipango yake kwa sasa.

Leave A Reply