The House of Favourite Newspapers

Aharibiwa sura kwa maji ya moto kisa, kula chabo!

0

Naam tumekutana tena kwenye kona yetu mpya ya mzee wa Chabo. Nina imani unataka kujua wakati wa ujana wangu nilikuwa nafanya nini mpaka kubatizwa jina la Mzee wa Chabo, pia uso wangu kuwa na makovu na jicho moja kama Shetani japo sijamuona.

Jina langu naitwa Salmini Maulana, nina umri wa miaka 70. Najua utashangaa uso wangu umekuwa kama ukuta uliokosa lipu na nina jicho moja kama shetani wa kutumwa. Hii yote imetokana na ajali nilizokutana nazo kwenye mishemishe zangu za chabo wakati wa ujana wangu.

Uso wangu ulipata ajali mara ya kwanza kwa kumwagiwa maji ya moto kutokana na kutegewa kwa siku nyingi na watu waliochoka tabia zangu chafu za kuwachungulia kwenye starehe zao.
Sikuchoka baada ya kuuguza majeraha ya moto, nilipumzika kwa muda na kurudi tena kilingeni. Niliendelea na tabia zangu chafu za kutembea kwenye nyumba za wageni na kwenye nyumba za watu. Kila dirisha kulikuwa na matundu kwenye nyavu za mbu.

Leave A Reply