The House of Favourite Newspapers

Aika, Nahreel kuipeleleka light-up Nigeria

0

aika2

Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na vichwa viwili, Aika na Nahreel kwa mara ya kwanza linatarajia kuitambulisha shoo yao inayojulikana kama Light Up nchini Nigeria.

Akichonga na Showbiz Xtra, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo Aika alisema hadi sasa wamefanya matamasha sehemu tofauti jijini Dar na nje ambapo wanategemea hivi karibuni kwenda Nigeria kisha nchi zingine za Afrika.

“Tuko katika mipango ya mwisho kuelekea nchini Nigeria kwa ajili ya tour yetu ambayo tumekwisha ianza hapa nchini ya Light-Up, baada ya hapo tutazunguka pia kwenye nchi zingine za Afrika,” alisema Aika

Leave A Reply