The House of Favourite Newspapers

Ray, Millard Ayo, Ruby kujiunga na Shtuka Mapema

0

Mastaa kibao wakiwemo, Mtangazaji Millard Ayo, Mwanamuziki, Hellen George ‘Ruby’, Muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine kibao wanatarajiwa kujiunga na Kampeni ya Mimi ni Nani? Shtuka Mapema inayotarajiwa kufanyika Aprili 3, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Josam House, Mwenge jijini Dar.

Akizungumza na Amani, mratibu wa tamasha hilo, Harris Kapiga alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwakusanya wale wote kuanzia waliomaliza kidato cha nne na hawakufanya vizuri kisha kuwapa somo la kutokata tamaa, kwanza wajitambue wao ni kina nani na pili waweze kushtuka mapema.

“Tunatarajiwa kuwa na mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda sambamba na Lilian Mwasha na Angel Magoti ambapo mbali na hiyo tamasha hilo ni kuwainua wote waliokata tamaa ya maisha waweze kujitambua mapema,” alisema Harris na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa ni 5,000 kwa watu wawili.

Tamasha hilo limedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na  Global Publishers.

Leave A Reply