The House of Favourite Newspapers

Airtel Money Yaja na TESA KIMILIONEA Wateja Kujishindia Mamilioni na Magari

0
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano (kushoto) na Mkurugenzi wa Airtel Money, Isaac Mchunda wakizindua promotion hiyo.

 

 

DAR ES SALAAM, Alhamisi 10 Februari 2022: Airtel Tanzania, ambayo ni kampuni tanzu ya Airtel Afrika na kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano pamoja na  huduma za fedha kupitia simu za mkononi iliyoenea  katika nchi 14 Barani Afrika, leo imetangaza kuzindua promosheni mpya kupitia huduma yake ya Airtel Money itakayodumu kwa  miezi mitatu ambapo wateja wa Airtel Money wataweza kujishindia zawadi kabambe.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano akizungumza kwenye uzinduzi huo. 

 

 

Promosheni hiyo inayoitwa TESA KIMILIONEA inawapa Watanzania fursa ya kujishindia Tzs 100,000, Tzs 1 milioni au zawadi kubwa ya Tzs 10 milioni na vilevile zawadi ya gari mpya aina ya IST moja kila mwezi.

 

Wateja na Mawakala wanaotumia huduma za Airtel Money mara kwa mara ndio watkaopata nafasi ya kuingia kwenye droo na kuwa na bahati ya kujishindia zawadi kwenye droo za wiki na mwezi.

 

Kuingia kwenye droo, wateja na mawakala watahitajika kutumia moja ya huduma hizi, kuweka pesa, kutuma pesa Airtel kwenda Airtel, kutoa pesa, kulipia bili kwa kutumia huduma ya Airtel Money, kufanya miamala ya kibenki, huduma za kutuma pesa nje ya nchi, kununua bando na kununua muda wa maongezi na kwa mawakala ni kuweka na kutoa pesa.

Mkurugenzi wa Airtel Money, Isaac Mchunda akizungumza kwenye uzinduzi wa promotion hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano.

 

 

Kupata fursa hii, wateja watahitajika kupiga *150*60# na kufanya miamala au kufanya miamala kuptia Applikesheni ya Airtel.

 

Miamala yote ya Airtel Money itaingia kwenye droo ya wiki, na kutakuwa na washindi 100 ambao watajishindia Tzs 100,000 kwa kila mmoja na wengine wawili wa kila wiki kujishindia Tzs 1 milioni kwa kila mmoja.

Vile vile, miamala yote kwa kila mwezi watakuwa na nafasi ya kujishindia zawadi kubwa ya Tzs 10 milioni kwa kila mmoja au gari mpya Toyota IST kwa mshindi mmoja.

 

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema: “Sisi Airtel Money tumedhamiria kuwahudumia na kuwazawadia wateja wetu.

 

Promosheni hii ni moja ya mfano wa vile tunaongeza dhamana kwa kurudisha kwa wateja wetu na kuongeza hamasa jinsi ya kutumia Airtel Money kwa matumizi mbalimbali. Nawatakia kheri wateja wetu wote.

“Kwa malengo yetu ya muda mrefu, tumekuwa tukiwekeza kwenye upanuzi wa mtandao kwa kuongeza idadi ya maduka yetu ya Airtel Money Branches pamoja na mawakala, na vile vile kuzindua matumizi ya applikesheni na kuendelea kuwekeza kwenye upanuzi wa mtandao wa 4G ili kufikia maeneo mengi ya Tanzania.

 

Kwa kuwekeza kwenye upanuzi wa mtandao pamoja na ubunifu wa bidhaa na huduma zetu, wateja wataendeleo kupata huduma zilizo bora hapa nchini.”

Leave A Reply