The House of Favourite Newspapers

Unganishwa na simu za “Bure na Halisi Kutoka Airtel”

0

airtelMkuu wa kitengo cha Internet Airtel Gaurav Dhingra akionyesha simu zinazopatikana kwenye maduka yote ya Airtel katika ofa iliyozinduliwa hivi karibuni kufuatia tamko la serekali la kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016. Simu hizo zinauzwa kwa gharama nafuu kabisa.


• Simu za Bure zinapatikana katika maduka yote ya Airtel

•Utapata vifurushi vinavyodumu kwa muda wa miezi minne na muda wa maongezi zaidi ya dakika1000

Dar Es Salaam, 14 Juni 2016, Kufuatia tamko la serikali la kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016, Airtel Tanzania imeanzisha ofa kabambe ya “simu za bure na halisi” zinazopatikana katika maduka yote ya Airtel. Tangazo hilo limesema kwamba simu za Bure na halisi zinapataikana kwa wateja wote wenye simu bandia na  ambazo sio za viwango vinavyokubalika  katika soko la Tanzania  , kwa kununua kifurushi chenye dhamani  ya sh. 22,000 / = Tshs tu.   Simu hizi za bure na halisi zinazotolewa  na Airtel ikiwemo  ITEL 2090 na FERO 180, zikiwa na dakika  550  kwa kupiga mitandao yote, zenye ujumbe mfupi 3000 na 250 MB kwa muda wa miezi minne.

Akitoa maoni yake juu ya ofa hii, mkuu wa kitengo cha  Internet Airtel Tanzania, Gaurav Dhingra alisema “tunatambua kwamba baadhi ya wateja wetu  bado wanatumia simu ambazo hazina uhalisia, hivyo wako katika hatari ya kuzimiwa simu zao hapo itakapofika siku ya Alhamisi, Juni 16. Kuwasaidia Wateja kuweza  kununua simu zenye kiwango kinachokubalika, tumeamua kutoa simu zenye uhalisi katika gharama nafuu kabisa  zenye vifurushi  vitakavyoduma kwa muda wa miezi minne.  

Kwa kuongezea, tuna simu za aina tofauti tofauti ambazo ni smartphone kwa kuwapa wateja wetu uwezo wa kuchagua zaidi kama vile Magnus Z11, Huawei Y3C na Techno W3  ambapo mteja atapata kifurushi chenye dakika zaidi ya 1000. Hivyo basi , mteja wetu wa Airtel mwenye simu iliyo bandia anatakiwa kufika kwenye duka letu lolote la Airtel na simu yake ili aweze kununua simu yenye kiwango kinachokubalika. “alinukuliwa Dhingra

Wateja wa Airtel wanaweza kuhakikisha kama simu zao ni bandia au la, kupiga *#06# au kutembelea mawakala katika maduka ya Airtel lililokaribu nae.

 

Leave A Reply