The House of Favourite Newspapers

Vodacom yawatoa wasiwasi wateja wao

0

Zikiwa zimebakia siku mbili tu simu feki kuzimwa nchini kote, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Imewahakikishia wateja wake kwamba fedha zao zote zitakazokuwa kwenye simu kupitia mtandao wa M-PESA watoe shaka kwani pesa zao zitakuwa salama kabisa na vilevile hata kadi zao za simu zitakuwa na usalama wa hali ya juu ila wafanye haraka kununua simu za bei nafuu kabisa kuanzia shilingi elfu 18/-zilizopo katika maduka ya kampuni hiyo ambayo yamesambaa nchi nzima.

Aakiongea na kituo hichi Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia alisema katika kutekeleza agizo la Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) la kuzitaka kampuni za mawasiliano kutoa elimu kwa wateja wao kuhusiana na simu zisizokuwa na kiwango yaani simu feki.

Vodacom Tanzania kesho itaendeleza kampeni maalum ya uhamasishaji wa huduma zake mbalimbali ikiwemo kusajili laini kwa wateja kwa njia ya kieletronikali pia kuwauzia wateja simu halisi na za gharama nafuu nchi nzima.

SIKILIZA AUDIO HAPA

Leave A Reply