The House of Favourite Newspapers

Airtel na Letshego Wawajaza Mkwanja Washindi wa Kuza Akiba na Ushinde Droo ya 4

0
Meneja Matukio wa Aitel, Dangio Kaniki akimpigia mmoja wa washindi wa droo hiyo kumpasha kuwa ameibuka mmoja wa washindi katika washindi 25. Kulia ni Neema Tatock kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha aliyekuwa akisimamia uchezeshwaji wa droo hiyo.

 

 

 

WATEJA wa Benki ya Letshego na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel, leo Jumatano wameondoka na mkwanja kiulainiii baada ya kuibuka kidedea kwenye promosheni ya Kuza Akiba na Ushinde ambapo droo ya nne ilichezeshwa na jumla ya washindi 25 waliondoka na mkwanja.

Akizungumza kwenye hafla ya kuchezesha droo hiyo, Meneja Matukio wa Aitel, Dangio Kaniki amesema hiyo ni promosheni ya tatu ambapo wameendelea kumwaga mkwanja wa wateja wao wakishirikiana na Benki ya Letshego.

Wachezeshaji wa droo hiyo wakiangalia kwenye luninga jinsi jina la mshindi linavyopatikana kwenye droo hiyo inayochezeshwa kidigitali.

 

 

 

Dangio amewashauri watumiaji wengine wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Airtel na kushiriki kwenye promosheni hiyo ambapo mshindi katika droo ya mwisho anatarajiwa kujizolea kitita cha shilingi milioni tano.

Katika droo hiyo washindi 25 walipatikana ambapo walipigiwa simu na kukabidhiwa pesa hiyo papo hapo.

Meneja Masoko wa Benki ya Letshego, Uswege Mwaipyana (kulia) akiweka kumbukumbu za droo hiyo kimaandishi.

 

 

 

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Benki ya Letshego, Uswege Mwaipyana amesema benki yake inaendelea kushirikiana na Airtel kumwaga mapesa kwa ajili ya washindi wa promosheni hiyo.

Uswege amewataka wateja wa Aitel na Letshego kuendelea kushiriki promosheni hiyo ambapo droo ya mwisho ina zawadi kubwa tatu ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na pesa taslimu milioni tano, wa pili milioni mbili na nusu na wa tatu ataondoka na milioni moja.                                            HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/ GPL  

Leave A Reply