The House of Favourite Newspapers

Airtel Yakabidhi Vitabu Shule ya Sekondari Mazinde Day-Korogwe‏

0

Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Aluta Kweka ( kulia) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa (wa kwanza kushoto) akifatia na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Patricia Andrew Mbigili (katikati) wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya mazinde Day wakionyesha vitabu walivyokabidhi na Airtel ikiwa na lengo la kutatua changamoto ya uhaba wa vitabu shuleni hapo. Vitabu hivyo vya sayansi vinathamani ya shilingi milioni 3.

Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Aluta Kweka akimkabidhi vitabu vya sayansi mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mazinde Day, Bi Jermana Mchome (katikati) ikiwa ni msaada katika kuendeleza elimu na kutatua changamoto za uhaba wa vitabu shuleni hapo. Akishuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa.

Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Aluta Kweka (kushoto) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Korogwe ,Hafsa Mtasiwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Mazinde Day, Jermana Mchome (katikati) wakionyesha vitabu walivyokabithi na Airtel ikiwa na lengo la kutatua changamoto ya vitabu shuleni hapo. Vitabu hivyo vya sayansi vinathamani ya shilingi milioni 3

Leave A Reply