The House of Favourite Newspapers

Airtel Yaondoa Tozo Kwa Watumiaji wa Airtel Money

0
Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money, Isack Nchunda akiielezea huduma hiyo mpya kushoto ni Meneja uhusiano wa Airtel, Jenipher Mbuya.

 

DAR ES SALAAM: Julai 1 2022; Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imeendelea kufanya huduma zake za Airtel Money kuwa nafuu kwa kuendelea kuhimiza matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi kwa watumiaji wa Airtel Money kwa kuzindua tumia Airtel Money Bila Tozo.
Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Isack Nchunda (mbele kulia) na wafanyakazi wa Airtel walivyoizindua huduma hiyo.
Taarifa hii kabambe ya Airtel Money Bila Tozo imetangazwa leo na Airtel huku ikiishukuru serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake iliyochukua hivi karibuni ya kuweka punguzo la tozo kwa miamala yote inayofanya kupitia  simu za mkononi, Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Isack Nchunda alielezea jinsi Airtel ilivyojipanga kuendeleza dhamira hiyo kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya kurahisisha gharama za kufanya miamala ya simu za mkononi kwa kubainisha kuwa Airtel itaondoa gharama ya tozo kwenye kutuma na kupokea fedha kwa kiwango cha hadi kufikia 29,999 Airtel kwenda Airtel.
Nchunda aliongeza kuwa wateja wengi wa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi hawana akaunti za benki, na kiwango chao cha kutuma au kutoa fedha huwa mara nyingi ni mpaka 29,999. Kwa punguzo la tozo kwenye kutuma na kutoa kutawafanya wateja wa Airtel kutuma na kutoa fedha bila ya maumivu ya tozo. Hivyo kutawafanya wateja wa Airtel na hasa wenye kipato cha chini kufanya miamala yao kwa unafuu na kwa Uhuru zaidi.
Vile vile, kwa mteja wa Airtel anayetumia Applikesheni ya Airtel Money kwa kutuma fedha Airtel kwenda Airtel, ataokoa grama za tozo kwa karibia viwango vyote.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza promosheni hii, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema “Tunatangaza leo Airtel Money Bila Tozo, hatua hii ya Airtel Money kuondoa tozo inalenga kuhimiza na kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa mtandao  baada ya kujidhihirishia jinsi huduma za fedha kidigitali zinavyobadilisha maendeleo ya uchumi kwa wananchi.
Nchunda aliongeza kuwa Airtel wanayo Imani kuwa promosheni hii ya Airtel Money Bila Tozo itawafanya Watanzania kuendelea kufanya miamala kwa Uhuru na kuchagua Airtel Money kuwa changua lao kwenye huduma za simu za mkononi pale wanapotaka kufanya miamala ya fedha kwa kutuma na kutoa pesa Bila Tozo kwa kutumia Airtel.
 “Promosheni ya Airtel Money Bila Tozo itaendelea kuimarisha biashara nchini na kufanya malipo kuwa nafuu na rahisi kwa kujenga mazingira bora na nafuu ya kila huduma jumuhishi kupitia huduma hii ya pesa kwa njia ya mtandao kwa wateja wote wa Airtel Money na hata wale ambao  hawajafikiwa na huduma za kibenki. Airtel  tutawahudumia  wote kupitia Airtel Money kwa kuwa huduma zetu zimefika kila mahali kwa lengo la  kutoa fursa ya huduma kwa kila anaehitaji  huduma za kifedha kwa kufanya malipo au kutuma na kutoa fedha” alisisitiza Nchunda.
Nchunda asema kuwa ili Airtel kuendelea kuwahudumia Watanzania vizuri zaidi, Airtel inaendelea kuwekeza kwenye ubunifu wa bidhaa pamoja na kupanua wigo wa miundo mbinu ya usambazambaji ya Airtel Money ili kutoa huduma bora ya fedha kwa simu za mkononi hapa nchini Tanzania. Tunayo furaha ya kuwa na maduka ya Airtel Money zaidi ya 3,000 nchini kote ambayo yanatoa huduma  sawa na mawakala wetu zaidi ya 150,000 walio sambaa nchi nzima.
“Tutaendelea kutoa huduma ya hali ya juu kwa wateja wetu ili kuhahakisha wateja wanapata huduma iliyo bora, inayopatikana kwa urahisi na nafuu popote pale walipo kwa masaa 24 siku saba za wiki wakiwa popote au wanapokuwa kwenye biashara zao”. Alimaliza kusema Nchunda.
Leave A Reply