The House of Favourite Newspapers

Airtel yashinda tuzo mbili kwa kutoa huduma bora kwa wateja‏

0

pic 1 (3)MKurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso akipokea tuzo ya ubora katika kipengele cha kutoa huduma za kimtandao kutoka kwa waandaaji wa tuzo za Tanzania Leadership Award bwana Kishore Bollakpalli (kushoto). Airtel Tanzania imejishindia tuzo mbili za ubora katika kipengele cha kutoa huduma za kimtandao pamoja na huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja.

Yajishindia tuzo kwa matumizi bora katika kutoa huuduma za kimtandao pamoja na huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja

Dar es Salaam, Jumanne 15th December 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma za kibunifu imetunikiwa tuzo mbili za ubora za Tanzania Leadership Awards 2015 katika halfa iliyofanyika katika hotel ya Hyatt jijini Dar es salaam.

Airtel imejishindia tuzo hizo katika kipengele cha matumizi bora ya huduma za kimtandao kufikia wateja wake (best use of social Media in marketing) pamoja na kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja (brand excellence) katika sekta ya mawasiliano na kuwashinda makapuni mengine yaliyokuwa wakichauana nayo katika kinyanganyiro cha tuzo hizo

Wakionge wakati wa kukabidhi tuzo hizo , waandaaji wa tuzo hizo za Tanzania Leadership Awards, Bwana Kishore Bollakpalli alisema ” Airtel imepata tuzo hizi kutokana na kufanya vizuri zaidi katika kuwasiliana na wateja wake kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii na hivyo kuwafikia wateja wake nchini nzima kwa urahisi zaidi.

akini kwa upande wa tuzo ya Brand excellence, Airtel imeonyesha kwa vitendo dhamira yao ya kutoa huduma bora kwa wateja wake huku ikitoa bidhaa na huduma za kibunifu ili kukidhi mahitaji ya wateja wake na kuboresha maisha yao.

Akipokea tuzo hizo Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwana Sunil Colaso alisema” Tunayofuraha kupokea tuzo hizi za Tanzania Leadership award na tunaamini huu ni ushuhuda kamili unaoonyesha kwa vitendo dhamira yetu ya kutoa huduma zenye zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu zikiwemo huduma za intaneti, huduma za kifedha kupitia simu za mkononi na kuchochea kukua na upatikanaji wa huduma za kifedha nchini”.

Colaso aliongeza kwa kusema Airtel itaendelea na dhamira yake yakutoa huduma zinazogusa mahitaji ya wateja wake u na kuwaweka karibu ili kuendelea kutoa huduma bora zaidi katika miaka ijayo.

Tuzo za Tanzania Leadership Awards zinalenga kutambua na kupongeza jitihada zinazofanya na watu binafsi na makapuni katika kuboresha uchumi wa Tanzania na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Leave A Reply