The House of Favourite Newspapers

AJALI MBAYA… DEREVA WA NAPE AFICHUA MAZITO

BAADA ya hivi karibuni kupata ajali mbaya ya gari, dereva wa Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, Michael Sangu ‘Mike’ ameibuka na kuanika mazito, Ijumaa linakupa habari kamili.

 

Akizungumza na IJUMAA, Mike ambaye pia ni msanii wa filamu za Kibongo alisema kuwa gari lilikuwa kwenye mwendo wa kawaida lakini walijikuta wakipata ajali ikiwa ni baada ya gari kugonga kwenye shimo kutokana na changamoto ya barabara kwani ni mbaya sana.

 

Mike aliendelea kueleza kuwa baada ya gari kugonga shimo hilo, lilipasuka tairi mbili za kushoto ikasababisha gari kuyumba na kupinduka. “Tulikuwa kwenye mwendo wa kawaida tu lakini kutokana na changamoto ya barabara kuwa mbaya gari liligonga shimo na kupinduka.

 

“Eneo la ajali pale ilionekana kwamba tairi mbili za kushoto zimepasuka, kwa kweli ile ilikuwa ajali mbaya sana ila tunamshukuru Mungu tulitoka salama, yaani ni Mungu tu kwa kweli. “Niliumia  kidogo shingo na bega lakini kwa sasa ninaendelea vizuri na hakuna mtu aliyeumia sana ni maumivu madogomadogo tu,” alisema Mike.

Kwa upande mwingine Mike alimshukuru bosi wake, Nape kwani  alimwelewa kutokana na ajali hiyo kwa sababu alimwelewa kwamba ni bahati mbaya na uzuri wakati inatokea alikuwa anaona. “Namshukuru sana bosi wangu Nape kwani ni mtu mzuri na kwa muda wote aliofanya naye kazi amekuwa akiwathamini sana wafanyakazi wake,” alisema Mike.

 

MAAJABU YA AJALI

Kwa upande mwingine Mike alieleza kuwa ajali hiyo ilikuwa na maajabu kwani baada ya kutokea ilionekana tairi zimepasuka lakini walipoenda kujaza upepo hakuna sehemu yoyote iliyoonekana kuwekwa kiraka.

“Ilinishangaza sana kwa sababu katika eneo la ajali tairi zilionekana kwamba zimepasuka lakini zilipoenda kujazwa upepo hakuna iliyokuwa na panja hata moja na hazikuwekwa kiraka chochote,” alimaliza Mike.

 

Septemba 24, mwaka huu Mbunge Nape akiwa na watu wengine kwenye gari lake aina ya Land Cruiser VX walipata ajali katika Kijiji cha Kibutuka wilayani Liwale mkoani Lindi, ambapo walikuwa wakielekea Liwale kuhudhuria mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa.

STORI:GLADNESS MALLYA NA HAMIDA HASSAN, IJUMAASaid Ally, Dar es Salaam

UCHAWI!! MANARA Amlipua Ajibu Imani za Kishirikina

Comments are closed.