The House of Favourite Newspapers

Ajali Mbaya: Prado Lagonga Lori Pwani, Mpishi Maarufu Lilian Catering Afariki… -Video

0

Mpishi maarufu wa vyakula na mpambaji kwenye shughuli mbalimbali mwenye makazi yake mkoani Morogoro anayejulikana kwa jina maarufu la Lilian Catering amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea leo asubuhi maeneo ya Chamakweza mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa mashuhuda eneo la tukio wameiambia Global TV kuwa Lilian ameaga dunia baada ya gari alilokuwemo aina ya Toyota Prado lililokuwa likitokea mkoani Dar es Salaam kuelekea Morogoro kugonga lori lililokuwa limepaki pembezoni mwa barabara baada ya kupata hitilafu.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, ACP Pius Lutumo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari dogo aina ya Prado.

Leave A Reply