The House of Favourite Newspapers

Bondia Aliyeriki Dodoma Kwa Kipigo, Familia Yaibua Utata

0
Ibrahim Najum enzi za uhai wake.

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Najum kutoka Mbeya amefariki juzi mchana katika hospitali ya rufaa ya Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya pambano lake Larent Segu huku familia yake kikana bondia huyo kupigwa na mke wake jambo ambalo halina ukweli.

Najum alilazwa katika hospitali ya Dodoma kutokana afya yake kutetereka kufuatia kudondoka ulingoni katika pambano hilo kabla ya kukimbizwa hospitali y Rufaa Dodoma kwa ajili ya matibabu ambapo juzi mchana aliaga Dunia.

Akizungumza kaka wa marehemu, Juma Mwakalebela alisema kuwa ni kweli mdogo wake amefariki kutokana na mchezo wa ngumi siyo kupigwa na mke wake kwani marehemu hakuwahi kuwa na mke hali iliopelekea kuzuka utata kijijini kwao kutokana na taarifa hizo.

“Ni kweli Ibrahim Najum amefariki na mimi ni kaka yake nipo hapa msibani (Kyela) tumeshafika kutoka Dodoma, Ibrahim amefariki kutokana na mchezo wa ngumi kwa sababu kilichotokea kila mmoja aliona pale na kama familia tunaelewa kwamba kilichotokea kimetokana na mchezo wa ngumi, tunajipanga na mazishi siku ya Jumamosi (leo).

“Lakini juzi wakati tupo njiani kuja huku Kyela nilishangaa kuwepo kwa taarifa kwamba Ibrahim alikuwa amepigwa na mkewe kabla ya kwenda Dodoma kwenye pambano siyo kweli kwa sababu hakuwa ameoa na alikuwa ana wanawake wawili mmoja ameanza naye na hakuna ambaye alikuwa akiishi naye sasa mambo ambayo yanasemwa na huko hayapo sawa natupa shida kiasi kinachopelekea mambo ya ushirikana baina ya ndugu na wanawake waliokuwa wa marehemu ambao tupo nao msibani,” alisema Mwakalebela.

ITAKULIZA! BABA ALIYEPATA AJALI ya NOAH na FAMILIA YAKE ASIMULIA WALIVYOSOMBWA na MAJI…

Leave A Reply