The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Ajali ya Treni na Coaster Yaua Wanafunzi Morogoro

Ajali ilivyotokea, wananchi wakihamaki.

MWANAFUNZI mmoja amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajali mbaya ya basi la abiria aina ya Coaster lililobeba wanafunzi na raia kugonga treni katika eneo la TANESCO, Morogoro Mjini.

Hali ilivyokuwa eneo la tukio.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri ambapo Coaster lilikuwa limebeba wanafunzi wengi wa Shule ya Sekondari ya Kayenzi waliokuwa wakienda shuleni pamoja na raia wachache lilipokatiza kwenye njia ya treni na kuligonga.

Taharuki eneo la tukio.

Imeelezwa pia kuwa treni lililiibuiruza Coaster hiyo kwa umbali wa mita 30 kabla ya kusimama hivyo kusababisha vifo hivyo na majeruhi.

Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu ya Global Publishers.

NA DUSTAN SHEKIDELE | GPL | MOROGORO

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

VIDEO YA TUKIO

 

Comments are closed.