The House of Favourite Newspapers

Ajali yaua watu 42 Ufaransa

0

8

Baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo wakipatiwa huduma ya kwanza.

TAKRIBANI watu 42 waliokuwa wakienda kutalii wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori katika barabara moja kusini magharibi mwa Ufaransa kisha magari yote kuungua kwa moto.

majeruhi

Ajali hiyo imetokea karibu na Puisseguin eneo la Gironde mashariki mwa Bordeaux, muda mfupi baada ya basi hilo kuanza safari kutoka mji ulio karibu.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameandika kwenye Twitter kwamba serikali “imechukua hatua zote kushughulikia ajali hiyo mbaya”.

majeruhi 3

Mkasa huo ndio mbaya zaidi kutokea barabarani Ufaransa tangu ajali iliyoua watu 52 mwaka 1982.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ufaransa, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 07:30 saa za huko karibu na kijiji cha Puisseguin.

Abiria 41 walikuwa kwenye basi lililopata ajali. Dereva wa lori naye alifariki. Ni watu wanane pekee walionusurika huku watano wakiwa na majeraha.

majeruhi 2

Wengi wa waliokuwa kwenye basi hilo walitoka chama cha wazee kilicho katika mji wa Petit-Palais-et-Cornemps.

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijabainika.

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, pamoja na mawaziri wa masuala ya ndani na uchukuzi wanatarajiwa kutembelea eneo la hilo la ajali.

Credit: BBC

Leave A Reply