The House of Favourite Newspapers

Ajali Yaua Watu Wawili Iringa, Mwili wa Mwanamke Wakutwa Umeungua Moto-Video

0

 

Watu wawili ambao bado hawajafahamika majina yao wamepoteza maisha katika ajali iliyohusisha magari wawili aina Semitela Faw moja lenye usajili wa namba T 286 CKG na lingine lenye namba za usajili KDE 492K kugongana  Februari 24,2023 eneo la Nyololo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari lenye namba ya usajili T 286 CKG kupoteza muelekeo na kusababisha ajali hiyo.

 

Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni dereva wa gari lenye namba T 286 ambaye bado hajafahamika jina lake pamoja na mwanamke ambaye mwili wake ulikutwa umeungua na moto ambaye pia jina lake halijatambulika.

Leave A Reply