The House of Favourite Newspapers

Ajibu Aingia Kwa Dk Shika, Apeleka Shangwe Yanga SC

0
Dk Louis Shika.

MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga, Ibrahim Ajibu amemtu­mia bilionea wa nyumba za Lugumi, Dk Louis Shika kupeleka shangwe za ushindi wa mabao 5-0, Jangwani.

 

Yanga ilipata ushindi huo mnono dhidi ya Mbeya City mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

Katika mechi hiyo, ma­bao ya Yanga yalifungwa na Mzambia, Obrey Chirwa aliyepiga ‘hat trick’ huku Emmanuel Martin akifunga mawili.

Mshambuliaji tegemeo wa Yanga, Ibrahim Ajibu.

Akizungumza na Champi­oni Jumatano, Ajibu alisema katika mechi hiyo walistahili kushinda idadi kubwa ya ma­bao lakini matano waliyoyapata “im­ependeza zaidi.”

 

Ajibu alisema, mechi hiyo haikuwa nyepesi kama wana­vyohisi mashabiki, lakini juhudi na ku­jituma kwa wache­zaji huku wakifuata maelekezo ya kocha wao Mzambia, George Lwad­amina ndizo zimewawezesha wao kupata ushindi huo.

 

“Nadhani haya mabao ma­tano tuliyoyapata yamepen­deza zaidi, licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kufunga idadi kubwa ya mabao katika mechi hiyo.

 

“Idadi hiyo ya mabao kwa upande wangu naona imependeza, hivyo basi tujipange kwa ajili ya mechi ijayo dhidi ya Tanzania Prisons,” alisema Ajibu.

 

Imependeza zaidi ni msemo ambao umekuwa maarufu kwa siku za hivi ka­ribuni baada ya ku­tumiwa na Dk Shika wakati akitaka kununua nyumba za mfanyabi­ashara Said Lugumi hivi karibuni.

 

Shika ameingia mkata­ba wa kufanya matangazo na kampuni ya kubashiri matokeo ya Sokabet.

Leave A Reply