The House of Favourite Newspapers

TAMBWE AJIFUA KUWAKABILI PRISONS

0
Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi ya kukimbia kwa pamoja.
… Wakiendelea kufanya mazoezi ya kuimarisha viungo vya mwili
Kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali akionesha uwezo wake uwanjani.

STRAIKA wa Yanga Mrundi Amissi Tambwe, ameanza rasmi kujifua na kikosi chake cha Yanga tayari kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons, utakaochezewa katika Uwanja wa Azam Complex, Jumamosi hii.

 

Tangu mzunguko wa kwanza wa ligi umeanza, Tambwe hajafanikiwa kucheza hata mchezo mmoja kutokana na kusumbuliwa na goti, ambapo sasa anaonekana kupona na kurejea uwanjani kwa ajili ya kuitumikia klabu yake hiyo kwenye mchezo wao wa wikiendi hii.

 

Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kuwafunga ndugu zao Mbeya City mabao 5-0, katika mchezo uliochezewa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

 

Yanga iko nafasi ya tatu kwenye ligi, ikiwa na pointi 20 nyuma ya wapinzani wao Simba wenye pointi 22 sawa na Azam FC.

PICHA: MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

 

Leave A Reply