The House of Favourite Newspapers

Ajibu Awashika Pazuri Yanga SC

KIUNGO mshambuliaji anayeongoza kwa asisti nyingi Yanga, Ibrahim Ajibu, ameibuka na kuwaambia maneno ma­zuri ya kuwatia matumaini mashabiki wa timu hiyo, kwa kutamka kuwa mashabiki wasihofu, mambo mazuri yanakuja.

 

Kauli hiyo aliitoa ikiwa ni saa chache kabla ya pambano lao dhidi ya Mbao FC ka­tika mchezo wa Ligi Kuu Bara jana Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Cham­pioni Jumatatu, Ajibu alisema wao kama wache­zaji wanatambua umuhimu wa mashabiki wao, hivyo ni lazima wapate matokeo mazuri katika michezo ijayo ya ligi ili kuhakikisha wana­fanikisha malengo yao.

 

Ajibu alisema, wanafa­hamu ugumu wa ligi uliopo katika msimu huu, lakini watahakikisha wanafanya kila liwezekanalo ku­fanikisha ushindi huku akiwataka mashabiki kuto­kata tamaa kuji­tokeza uwanjani, pale wanapopata matokeo mabaya.

 

“Tunataka kuona timu yetu ikiendelea kupata matokeo mazuri,” alisema Ajibu.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam.

MABAO YOTE YA YANGA VS MBAO FC 2-0 (VIDEO)

Comments are closed.