The House of Favourite Newspapers

Ajibu: Nisemeni Tu Mi Mvivu, Wala Siumii

0
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu.

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu ameanika wazi kwamba huwa hakasiriki kutokana na kuitwa mvivu wa mazoezi kutokana na kuwa na malengo ambayo anajiwekea na anayafi kia.

 

Kiungo huyo ameweka bayana kwamba kwake amekuwa akishukiwa kwamba amekuwa mvivu wa mazoezi tangu anaanza kucheza soka lakini amekuwa na kiwango cha juu na timu nyingi amekuwa akianza kikosi cha kwanza.

 

Nyota huyo ambaye msimu uliopita alikuwa Yanga amesema kwamba hata akiitwa kwamba ni mvivu kwake hakasiriki kwa sababu anajitambua wapi shabaha yake ilipo.

 

“Tangu naishi kwetu nimekuwa naambiwa mvivu, lakini mimi najua ninachokifanya na najua shabaha yangu wapi nalenga.

 

“Wala sikasiriki kuitwa hivyo kwani nimekuwa naambiwa tangu nakaa nyumbani hadi sasa nakaa kwangu, lakini nafanya mazoezi yangu na nafata kile ambacho naambiwa na makocha wangu,” aliweka wazi kiungo huyo.

Stori: Said Ally, Dar es Salaam

Leave A Reply