The House of Favourite Newspapers

AJISALIMISHA POLISI BAADA YA MAHINDI ALIYOIBA KUNASA MABEGANI – VIDEO

KIJANA Frank Japhet (23), mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, amelazimika kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 20, anaodaiwa kuuiba kung’ang’ania mabegani.

 

Wakati akihojiwa kituoni hapo, mtuhumuwa huyo amesema mzigo huo, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la Mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, mkoani Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo Mei 3, 2018, akaongeza kwamba aliondoka na mzigo huo hadi eneo la Stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, ambapo mzigo huo uling’ang’ania kichwani.

Ameendelea kusema kwamba alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani! Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu, alidai alichoka hivyo akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi.

Japhet mpaka sasa yuko Kituo cha Polisi Mlandizi na mzigo wake kichwani akisubiri mwenye mali aliyoiiba na Jeshi la Polisi Mlandizi tayari limemuita afike kituoni hapo. Tutawaletea taarifa zaidi za tukio hilo.

Mtandao wa www.globalpublishers.co.tz umempigia Mkuu wa Kituo cha polisi kuzungumzia tukio hili na haya ndiyo yalikuwa majibu yake:

“Mimi siyo msemaji wa Jeshi la Polisi, mtafute Kamanda wa Polisi (RPC) atakueleza kila kitu, kama atakosa mtafute hata msaidizi wake.”

Baada ya kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwanai, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna Warioba alisema:

“Ni kweli tukio hilo limetokea usiku wa kuamia leo, na hapa nipo kwenye kikao nikitoka tu nitafanya press (mkutano na wanahabari) kuhusu tukio hilo saa 7:30 mchana,” alisema Kamanda huyo.

Ohoooooooooo…… Mkazi wa Mbezi, Dar es salaam, Frank Japhet (23) amelazimika kujisalimisha kituo cha polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kg 20, anaodaiwa kuuiba kung’ang’ania kichwani. Kwa maelezo ya mtuhumuwa huyo aliyoyatoa kituoni hapo, mzigo huo wa mahindi, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo. Amesema, alipoondoka na mzigo huo hadi eneo la stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, mzigo huo uling’ang’ania kichwani. Amesema, alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani! Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu, alidai alichoka akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi. Mpaka sasa yuko kituo cha polisi Mlandizi na mzigo wake kichwani akisubiri mwenye mali aliyoiiba ambaye jeshi la polisi Mlandizi tayari limemuita afike kituoni hapo. Tutawaletea taarifa zaidi za tukio hilo.

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

MAAJABU: Mtanzania Anayehudumia Nyuki, Hawamng’ati

Comments are closed.