The House of Favourite Newspapers

Ali Choki Arudi Kwa Kishindo Na Extra Bongo Yake, Sasa Aja Na Penati Ya Mwisho

0
Ali Choki akitambulisha kurudi kwa bendi yake ya Extra Bongo alipokuwa akizungumza na wanahabari katika Ukumbi wa Andrewson leo.

Dar es Salaam, 21 Novemba 2023: Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ali Choki ‘Kamarade’ ukipenda Mzee wa Farasi leo ameibuka tena na Bendi yake ya Extra Bongo sasa hivi akiinogesha na jina la Baba Lao ambapo mwanamuziki huyo amesema anakuja na nyimbo kibao ikiwemo Penati ya Mwisho na nyinginezo na  sasa hakuna kulala tena ni mwendo mdundo mpaka kieleweke.

Mdau wa muziki wa dansi na mtangazaji maarufu wa habari za dansi, Hamis Dakota akizungumzia kurejea upya kwa Extra Bongo muda mfupi baada ya utambulisho huo.

Ali Choki ambaye miaka kadhaa iliyopita aliamua kuivunja bendi hiyo na kujhihusisha na mambo yake mengine sasa amerudi tena na bendi hiyo ambapo amesema itafanya uzinduzi rasmi Desemba 2 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Andrewson zamani ukiitwa T Garden uliopo Sinza Lion Jijini Dar.

Super Nyamwela (kulia) akifuatiwa na Super Benja walipokuwa kazini kwenye Extra Bongo ya kipindi hicho.

Choki katika kuinogesha bendi hiyo sasa hivi atakuja na chipukizi wengi wenye mawazo ya kileo zaidi ili kuwateka vijana na kuchanganyia na wakongwe wachache kwa ajili ya kuchanganya radha.

Kiongozi mstaafu wa Chama cha Muziki wa Dansi nchini, (CHAMUDATA) Hassan Msumari akielezea furaha yake kufuatia kurudi upya kwa Extra Bongo Baba Lao.

Ameendelea kusema kuwa katika uzinduzi huo kiingilio kitakuwa shilingi elfu kumi kawaida na meza maalum yaani (VIP) itakayosheheni vinywaji, minofu na asusa mbalimbali itakuwa shilingi laki mbili. Mwanamuziki huyo amesema katika ujio wa bendi anatarajia kutamba na wimbo wa penati ya mwisho na nyinginezo ambazo anaamini zitawashika mashabiki. HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS/ GPL

Leave A Reply