The House of Favourite Newspapers

Waarabu Waibeba Yanga Ligi ya Mabingwa Afrika, Kutua Algeria Kwa Kishindo

0

ALFAJIRI ya leo Jumanne, msafara wa kwanza wa kikosi cha Yanga, umesafiri kuelekea nchini Algeria kwa kutumia Ndege ya Shirika la Uturuki, tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao, CR Belouizdad.

Msafara huo wa kwanza, umeondoka na wachezaji waliokuwa hawapo kwenye majukumu ya timu zao za taifa, huku msafara wa pili wa wachezaji wanaocheza Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ukitarajiwa kuondoka kesho Jumatano baada ya kumaliza mchezo wa leo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zimebainisha kwamba, msafara huo wa kwanza umeondoka na Ndege ya Shirika la Uturuki, ambapo utapitia nchini Uturuki, kabla ya leo jioni majira ya saa 10 kutua Algeria.

“Leo (jana) asubuhi, kikosi kilifanya mazoezi ya gym, kisha kikajiandaa na safari ya kuelekea Morocco kupitia nchini Uturuki.

“Kundi la kwanza la wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wataondoka kesho (leo) saa 10 alfajiri kwa kutumia Shirika la Ndege la Uturuki, watapitia nchini Uturuki kabla ya kutua Algeria saa 10 jioni.

“Kundi la pili litaondoka tarehe 22 baada ya mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Morocco utakaochezwa kesho (leo) Jumanne.

“Ukiachana na msafara wa kwanza na wa pili, nyota wengine waliopo kwenye timu zao za taifa, Khalid Aucho (Uganda), Djigui Diarra (Mali) na Stephane Aziz Ki (Burkina Faso), wataungana na timu moja kwa moja huko Algeria baada ya kumaliza majukumu yao katika timu zao za taifa,” kilisema chanzo hicho.

Leave A Reply