The House of Favourite Newspapers

Alichoandika Prof. Mwandosya baada ya tetesi za kuhama chama chake

0

Mwandosya-Mark

Profesa Mark Mwandosya.

BAADA ya kuenea tetesi katika mitandao ya kijamii jana kuwa kuna baadhi ya viongozi wanampango wa kuhama vyama vyao akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya, hatimaye kiongozi huyo ameibuka na kuandika ujumbe kupitia akaunti yake ya Facebook.

Profesa Mwandosya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameandika hivi:

“Mitandao ya mawasiliano leo imesheheni tena taarifa za Profesa Mwandosya kuhama. Napenda kuwathibitishia ndugu, marafiki na Watanzania wenzangu, tena kwa ukweli kabisa, kwamba nahama, kutoka Dar es Salaam kwenda kijijini Lufilyo, Busokelo, Wilaya ya Rungwe. Karibuni sana kijijini.”

Leave A Reply