Maajabu Ndani ya Basi la Dar-Arusha-7

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

Nikaanza kuondoka kwa kasi huku mapigo ya moyo yakinienda mbio. Niliogopa. Ilibidi nitafute teksi ili inipeleke mjini, ghafla lile basi likanipita, abiria walitoa vichwa na kuniangalia, akiwemo yule mzee.

ENDELEA NAYO MWENYEWE…

Nilishtuka sana kuona vile. Ilibidi nifikiche macho nikiamini huenda ninachoona sicho. Yule mzee aliachia tabasamu laini huku akinielekezea mkono wake wa kulia wenye alama ya dole gumba.

Hapohapo, teksi ilipita, nikaisimamisha kunipeleka mjini. Nilimwomba dereva anipeleke kwenye hoteli yenye usalama wa ulinzi. Nilitamani kumweleza yaliyonipata lakini nikasita.

Nilipata hoteli, nikalala, asubuhi nikaelekea kwenye kazi zangu zilizonipeleka kule, sikuona ajabu yoyote ile. Nilirudi Dar kwa siku nilizopanga, nikapanda basi linalojulikana sana, nikafika Dar bila tatizo lolote.

Nilipofika Dar nilimsimulia mke wangu maajabu yote, akashangaa sana. Pia alinilaumu kwa kutomweleza kinagaubaga tangu nakwenda. Lakini alisema lazima mimi nilipanda basi la majini toka Dar mpaka Arusha. Nilikubaliana naye, nikamshukuru Mungu.

Lakini nimekuwa nikiamini kwamba, kumbe kuna baadhi ya haya mabasi yana maajabu. Tunatakiwa kumwomba Mungu hata kabla ya kutoka nyumbani kwenda stendi kusafiri.

Mwisho.

Loading...

Toa comment