The House of Favourite Newspapers

Alichokisema Freeman Mbowe Baada ya Akina Mdee Kutimuliwa Chadema – Video

0
Mwenyekiti, Freeman Mbowe.

 

RUFAA za Halima Mdee na wenzake 18 za kupingwa kufukuzwa uanachama na kamati kuu ya Chadema zimetupiliwa mbali na wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho.

 

Baada ya wajumbe hao chini ya Mwenyekiti, Freeman Mbowe kusikiliza rufaa hizo walizoziwasilisha ofisi ya Katibu Mkuu, Joh Mnyika, Mbowe alizungumza.

 

Pamoja na mambo mengine, Mbowe aligusia jinsi alivyotaka kuwasaidia wakati sakata lao la kusaliti, kughushi na kujipeleka bungeni kujiapisha kuwa wabunge wa viti maalum.

 

Mbowe alisema aliwasiliana na wazazi wa Halima ili wamsihi mtoto wao juu ya uamuzi alioufanya lakini ikashindikana.

“Nilipokuwa gerezani nilimwomba katibu mkuu (John Mnyika) amlete Halima, alikuja na (Ester Bulaya, niliwahisii sana.”

 

Akizungumza kwa uchungu, Mbowe amesema”niliwauliza nani aliwadanganya? Acheni huu ujinga!Nilimwambia kama unataka kazi niambiee nitakutafutia kazi hata nje ya nchi, utalipwa vizuri achana na ubunge.Nipo gerezani namuwaza Halima.”

 

Baada ya maelezo hayo, Mbowe aliwaongoza wajumbe wa kikao hicho kupiga kura kwa za wazi kwa kanda moja moja kwa wale wanaokubalia a na rufaa hizo ama kuzipinga.

 

Mwisho wa kura hizo, wajumbe walizitupilia mbali hivyo kuhitimisha suala hilo la uanachama ndani ya Chadema.

Kwa uamuzi huo wa Baraza Kuu na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Mdee na wenzake 18 wamepoteza sifa za kuwa wabunge wa Bunge la Tanzania.

 

Aidha, Mdee na wenzake wanayo fursa ya kwenda kupinga uamuzi huo wa Chadema Mahakamani ikiwa wana dhamira hiyo.

 

Mbali na Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha), wengine ni, waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu, Ester Bulaya na Esther Matiko pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

 

Pia wamo, Hawa Mwaifunga, aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bawacha (Bara); Agnesta Lambat, aliyekuwa katibu mwenezi na Asia Mwadin Mohamed, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Bawacha Zanzibar na Katibu Mkuu, Bawacha-Bara, Jesca Kishoa

 

Wengine ni, aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Nusrat Hanje, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Mtwara, Tunza Malapo.

 

Cecilia Pareso, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza, Felister Njau na Stella Siyao.

Leave A Reply