The House of Favourite Newspapers

Aliens wana tabia sawa na majini?

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA

Mpenzi msomaji wangu wiki iliyopita tuliona namna ambavyo barani Afrika viumbe wa ajabu waishio angani wa Aliens wanavyohusishwa na imani za kishirikina wakipewa jina la Kibwengo, Kinyamkera na Maimuna. Wengi wamekuwa wakihusisha viumbe hao na mambo ya ushirikina. Je, kuna uhusiano wowote kati ya Aliens na majini?

SASA ENDELEA…

Kwa wale wenye utamaduni au mazoea ya kusikiliza au kujisomea habari za UFO (Unidentified Flying Objects) au Aliens (watembezi/viumbe wanaofika hapa duniani kutoka sayari zingine), watakubaliana na mimi kwa kiasi kikubwa kabisa kwamba visa na matukio yanayoripotiwa ni kutoka ama Amerika ya Kaskazini (USA na Canada) na kwa uchache kabisa barani Ulaya.

Ni nadra sana kusikia hadithi za Aliens au UFO kutoka barani Afrika. Swali ambalo limekuwa likiulizwa na wengi ni kwamba ni kitu gani kimekuwa kinasababisha matukio haya yanajazana kwenye eneo moja? Ina maana hawa Aliens hawana data za kuchukua kwa wakaaji wa Afrika? Ina maana UFO hazina hata haja ya kushuka Tanzania?

Ili kuondoa taswira kuwa mada hii haina takwimu, kuna muhtasari wa matukio ya UFO kwa mwaka 2015 ambayo kwa Afrika ni Misri na Afrika Kusini pekee zinazoonekana kupata walau tukio mojamoja kwa mwaka mzima. Kwa takwimu, Marekani na Canada peke yake wana karibu 90% ya matukio hayo.

Kama tulivyoona kwa mataifa ya Magharibi, Aliens ni changamoto ya kiteknolojia lakini kwa Afrika ni ushirikina na mara nyingi mtu anapoona kiumbe wa ajabu hukimbilia kanisani kuombewa au kwa waganga ili azindikwe wakiwahusisha na majini au mashetani.

Kama ilivyo kwa Aliens, makabrasha ya Kiafrika yaliyoandikwa miaka mingi iliyopita yanaonesha kwamba viumbe hawa wameumbwa kwa moto na wamekuwepo hata kabla ya binadamu miaka lukuki iliyopita.

Maelezo hayo yanaonesha kwamba Aliens wana tabia sawa na majini kwani wana namna ya kuzaliana ili kuongezeka na pia hufa kama ilivyo kwa binadamu.

Pia kama ilivyo kwa majini, Aliens wana uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote wanalotaka, wanaruka na kwenda wanakotaka au kupita wanakotaka bila kutumia chombo chochote.

Si kila Aliens ana nia mbaya na mwanadamu japokuwa ni wakorofi na wanawaletea watu madhara ambayo hata hivyo, hayaelezwi ni yapi.

Kuna maelezo kwamba Aliens hujihusisha na mambo ya doria za angani. Aliens na majini wana sifa zinazofanana.

Tofauti kubwa iliyopo kati ya Aliens na majini ni kwamba majini wana maumbile maalum na wana uwezo wa kujibadilisha katika maumbile mbalimbali tofauti na sisi binadamu ambao tuna maumbile kamili ambayo hayabadiliki kwa maana ya kujigeuza. Zaidi sana maumbile yetu huongezeka au kupungua.

Aliens na majini wote wana uwezo wa kusafiri kwa kasi ya upepo kwa maana ya kufumba na kufumbua na kuelea angani bila chombo chochote.

Tofauti na Aliens, majini wao huwa wanakula mifupa na kinyesi cha farasi. Wengine wanakula moshi (ubani) na wengine wanapenda kunywa damu. Pia, tofauti na Aliens, majini hawaonekani kwa macho ya kawaida ila kwa utaalam maalum wanaojua binadamu wachache.

Kuna wanaoamini suala la viumbe hawa ni ndoto za wasiomwamini Mungu. Wanaamini kwamba kama kitu hakijaandikwa kwenye vitabu vitakatifu ni uwongo uliokithiri kwa sababu viumbe vyote aliviumba Mungu.

Wanaamini kuwa hakuna viumbe vingine zaidi ya binadamu, majini, wanyama na malaika. Nyingine zote ni stori za kutisha tu.

Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply