The House of Favourite Newspapers

Alisafiri mpokee basi ajue ulimmisi shosti

0

shutterstock_321381809Shangingi mie nimerejea tena leo na mada mpya kabisa, unaweza kuwa umeshajifunza kwa kungwi wako lakini kwangu ndiyo kwanza nagusia, hivyo usinichoke, wewe soma taratibu nikujuze mambo muhimu kwani wanawake wengi tukishaolewa ndiyo tunaona tumefika.

Wapo walioolewa na wanaume wanaofanya kazi za kusafiri, pia wapo ambao waume zao hupendelea kusafiri pale anapopata likizo ofisini kwake, shosti, mume akisafiri anakuwa amepata upenyo wa kupumzika na kelele zako nyumbani na za watoto wenu, sasa akiwa huko, andaa jinsi ya kumpokea ili ajue ulivyommisi, siyo anakuja anakutana na mambo yale yale aliyoyaacha wakati anakwenda likizo.

Shosti yeye kaenda likizo yake ya kiofisi na wewe ndiyo wakati wako wa likizo ili wote mkikutana muwe wapya na stress zote mmezitupilia mbali.

Nakusihi shosti wangu, ujipange ikibidi umtafute kungwi akufanyie masahisho kwa yale uliyosahau au akupe maujuzi zaidi, nia kubwa ikiwa tu ni kuipa uhai ndoa yako.
Asikwambie mtu, kuna wakati ndoa inachosha kwa sababu ya kuonana kila siku lakini mwenzako anaposafiri hujikuta unamkumbuka sana na kutamani arudi ili maisha yaendelee.

Ila kuna wanawake wengine huwa hawana muda na waume zao, anammisi lakini akirudi hata ile hali ya kummisi haioneshi anaongea naye kama vile walikuwa wote sikuhappy-coupleRafiki yangu, shosti wangu, mume ukimuonesha mapenzi yaliyopitiliza, hawezi kukuacha na wakati huo ndiyo wakati wa kumuonesha kuwa unampenda, unaweza kumuandalia chakula kitamu ambacho anapenda kula, ambacho huwa unakipika kwa nadra ili aelewe umuhimu wa siku hiyo.

Muandalie nguo za kuvaa baada ya kuoga akitoka safari, hii siku inakuwa ni spesho kwani najua si kawaida ya wanawake wengi kuwaandalia waume zao nguo kwa sababu na wao wanachohisi, lakini siku hiyo ifanye spesho kwa kumuandalia na kama anarudi usiku basi iwe nguo ya kulalia.

Yaani siku hiyo fanya vitu vipya kwake ambavyo vitakuwa kama sapraizi na baada ya hapo sasa muandae kwa faragha iwe ya uhakika isije kuwa faragha kama aliyozoea siku zote, hiyo iwe ya ‘baby came back’ kama ulikuwa ukichokachoka, siku hiyo usichoke bibi kwani hata yeye huenda akajiuliza umechoshwa na nani na yeye hakuwepo.

Leave A Reply