The House of Favourite Newspapers

AJIFUNGUA WATOTO WANNE KWA MPIGO, AMLILIA JPM – VIDEO

BINTI wa miaka 24, Radhia Solomon,  mkazi wa Mtaa wa Chemchemi, Magomeni-Mapipa jijini Dar es Salaam, ambae amejifungua watoto wanne kwa mpigo, amemlilia Rais John Magufuli; Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu; mawaziri na wote wanaoguswa  na tukio hilo, kumsaidia mahitaji muhimu ya watoto hao kutokana na hali yake ya maisha kuwa ngumu na kushindwa kuyamudu.

Akizungumza na Global TV Onlin, Radhia amesema ujauzito wake ukiwa na mwezi mmoja alianza kuugua tumbo na kwenda katika Hospitali ya Mwananyamala, jijini hapa, lakini baada ya kufanyiwa vipimo vya ‘ultra sound’, madaktari walimwambia kuna vitu hawavielewi, hivyo wakamweleza kurudi baada ya wiki moja na walipompima akakuta ana ujauzito wa watoto wanne.

 

Ameongeza kwamba madaktari wa Mwananyamala walimpa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuanza kliniki kwani hawakuwa na uwezo wa kumsaidia kulingana na hali yake. Muda wa kujifungua ulipofika alijifungua salama watoto wanne ambao wawili ni wa kike na wawili ni wa kiume na wote wanaendela vizuri.

 

Atakayeguswa awasiliane naye kwa namba 0682 604 202 ili kumsaidia mahitaji ya watoto wake ikiwa ni pamoja  na nguo, chakula, maziwa na mahitaji mengine madogo.

 

VIDEO: MSIKIE RADHIA AKISIMULIA ILIVYOKUWA

Comments are closed.