The House of Favourite Newspapers

Aliyekiri Kuhujumu Uchumi Ahukumiwa Jela, Faini Sh mil 100 – Video

MFANYABIASHARA Yasin Katare amehukumiwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulipa faini ya Mil.100 au kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukiri mashitaka ya utakatishaji fedha.
Mshitakiwa Katare yupo katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) Godfrey Gugai ambao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi.
Adhabu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo wakili wa utetezi, Shunde Mbutu aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu mshitakiwa kwa sababu ni kosa lake la kwanza.
Pia amedai kuwa ana familia inayomtegemea, amedai amekaa ndani mwaka wa pili na afya yake si nzuru kwani anaumwa na amekuwa akienda Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhudhuria kliniki.
Hakimu Simba amemuhukumu mshitakiwa kulipa faini ya Sh.Mil 100 kwa kuzingatia muda aliokaa gerezani muda mrefu na ni mgonjwa hivyo, wakimpa adhabu kubwa itaendelea kutesa familia yake.
Pia amesema, nyumba ya mshtakiwa itataifishwa na kuwa mali ya serikali na kwamba mshitakiwa akishindwa kulipa faini atatumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani.
Kwa upande wao Gugai na washitakiwa wenzake George Makaranga na Leonard Aloys wamesomewa mashitaka upya baada ya mashitaka matatu kati 43 ya awali kuondolewa na hivyo kubaki na mashitaka 40 na kati ya hayo 20 ni ya utakatishaji fedha na 19 ya kughushi ambapo baada ya kusomewa wamekana.
Katika mashitaka hayo mapya waliyosomewa 29 yanamkabili Gugai peke yake ikiwemo ya kupatikana na mali isiyo na maelezo ya Sh 3,634,961,105.02, huku Gugai na Makaranga wakishitakiwa kutakatisha fedha na Aloys na Gugai wanakabiliwa na mashitaka manane ikiwemo manne ya kughushi na manne ya utakatishaji fedha.

 

Comments are closed.