The House of Favourite Newspapers

Ally Niyonzima: Ninakuja Yanga SC

0

KIUNGO mkabaji wa Rayon Sports, raia wa Rwanda, Ally Niyonzima, amethibitisha kufuatwa na mabosi wa Yanga na kama dili likikamilika, basi haraka atasaini mkataba na kuja kukipiga Jangwani ndani ya msimu ujao.

 

Staa huyo wa Rwanda anayecheza namba sita ni kati ya wachezaji waliokuwa wanatajwa kuwaniwa na Yanga katika kuelekea msimu ujao kutokana na mapendekezo ya Kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael.

 

Mbelgiji huyo ametoa mapendekezo ya baadhi ya nafasi zifanyiwe maboresho, kati ya hizo, ipo ya kiungo mkabaji na Niyonzima ndiye alipewa nafasi kubwa ya kutua kuja kukipiga Yanga.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Niyonzima alisema kuwa meneja wake (jina lake amelifi cha) ndiye aliyefuatwa na viongozi wa Yanga (GSM) kwa ajili kufanya mazungumzo ya awali kujiunga na timu hiyo , ambayo yapo katika hali nzuri.

 

Niyonzima alisema kuwa hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kujiunga na timu nyingine itakayomhitaji kutokana na mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

 

Alisema kuwa kama akifanikiwa kujiunga na Yanga, basi anaahidi kuifanyia makubwa timu hiyo ikiwemo kuipa mafanikio mbalimbali ikiwemo ubingwa, kwani anaamini uwezo wake wa ndani ya uwanja.“Meneja wangu amenitaka niongeze mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha ninakuwa fi ti, kwani muda wowote nitajiunga na moja ya klabu kubwa Afrika, hivyo sijajua ni klabu ipi nitakayokwenda kuichezea.

 

“Kwani zipo baadhi ya klabu zilizoonyesha nia kubwa kuhitaji saini yangu, kati ya hizo ipo Yanga ambayo imeonyesha nia kubwa ya kunisajili baada ya viongozi wao kumfuata meneja wangu kwa ajili ya kufanikisha dili hili la usajili.

 

“Hivyo, kama mchezaji mimi ninaendelea kufanya mazoezi kwa nguvu zangu zote ili dili hilo likikamilika, basi nijiunge na Yanga nikiwa fi ti kwa ajili ya mapambano,” alisema Niyonzima.

 

Aidha, kiungo huyo alifungukia ukaribu kati yake na Mnyarwanda mwenzake anayekipiga Yanga, Haruna Niyonzima alisema kuwa hana undugu na nyota huyo, wao ni marafi ki wa karibu tangu walipojuana mwaka 2016/2017 wakiwa timu ya taifa ya Rwanda.

 

“Haruna siyo ndugu yangu kama watu wanavyofi kiria, zaidi ni marafi ki wa karibu sana na tulianza kujuana tukiwa katika timu ya taifa ya Rwanda, ni vema watu wakafahamu hilo,” alisema Niyonzima

Stori: Wilbert Molandi na Ibrahim Mussa,Dar

KWA UCHUNGU! MADAM RITHA KAONGEA kwa MARA ya KWANZA kuhusu KUMLIPA MSHINDI BSS..

Leave A Reply