The House of Favourite Newspapers

Ally Niyonzima wa Rayon Sports Asaini Azam FC

0

Azam FC wamekamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa kimataifa wa Rwanda, Ally Niyonzima, kwa mkataba wa miaka miwili.

Niyonzima aliyekuwa akicheza Rayon Sports ya Rwanda, usajili wake ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.

Kiungo huyo nyota mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba leo Jumamosi mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Niyonzima, ambaye yumo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam FC kwa ajili ya msimu ujao.

Usajili wa kwanza ulikuwa ni wa kiungo Awesu Awesu, kwa usajili huru akitokea Kagera Sugar.

Leave A Reply