The House of Favourite Newspapers

Amber Ruth: Mchungaji Mashimo Ni Kila Kitu Kwangu

0
Msanii wa Bongofleva, Rutyfiya Aboubakary ‘Amber Ruth’

Msanii wa Bongofleva, Rutyfiya Aboubakary ‘Amber Ruth’ leo Juni 6, 2021 amesema Mchungaji wa Kanisa la Emmaus Bible Church, Daudi Mashimo ndio kila kitu kwake kwa sababu amemtendea mambo mengi yaliyofanikisha kurudisha heshima yake ndani ya jamii.

Amber Ruth amefunguka hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Mapito kinachorushwa na Global radio na kuongeza kuwa mchungaji huyo amekuwa sehemu ya familia yake.

Mtangazaji wa kipindi cha Mapito, Zally Bebe akifanya mahojiano na Amber Ruth.

Amber Ruth na Mumewe Said Bakary, Septemba mwaka jana walihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya Sh milioni 11 au jela miaka 5 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa manne ikiwemo kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Aidha, inaelezwa kuwa Mchungaji Mashimo na wadau wengine ndio waliofanikisha kuwalipia faini hiyo na kuwezesha wawili hao kuwa huru.

Leave A Reply